Alhamisi, 6 Machi 2014

PICHA ZA LULU AKIWA KATIKA KABURI LA KANUMBA


 Jana ilikua ni siku ya kumbukumbu ya kifo ch amarehem Kanumba, ambae alikua anafikisha mwaka mmoja tangu alipofariki, mastar wa movie wengi walikuwepo katika kuhakikisha shughuli hiyo inaenda vizuri, ikiwa ni pamoja na kutembelea kaburi la Kanumba.

Lulu akilia juu ya kaburi la Kanumba 

Lulu na mama yake Kanumba

Irene Uwoya

Lulu katika kaburi la Kanumba

Lulu na mama yake 

GODFREY MGIMWA APOKELEWA KAMA MFALME KIJIJINI KWAO MAGUNGA


 Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa (kulia) akiwa  na bibi yake, Consolata Semgovano wakipungia mikono wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji alichozaliwa cha Magunga, Iringa Vijijini leo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Nyumbani  alikozaliwa babake na mgombea ubunge Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa, marehemu Dk. Mgimwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo.
 Msafara wa Mgimwa ukiingia katika Kijiji alichozaliwa cha Magunga.

 Mgimwa akisalimiana na wazee wa Kijiji hicho.


 Mgimwa akisalimiana na akinamama wa kijiji hicho.

 Mzee wa Kijiji cha Magunga akicheza kwa furaha wakati wa kumpokea Mgimwa 



 Ni nderemo nderemo kwa kwenda mbele ikiwa ni furaha ya wakazi wa kijiji hicho wakati wa kumlaki Godfrey Mgimwa.








 Mgimwa akijiunga kucheza na wanakijiji wenzie alipowasili katika Kijiji chao cha Magunga
 Msanii wa muziki wa kiszazi kipya na filamu, Ummy Wenslaus 'Dokii'akifanya vitu vyke katika mkutano huo wa kampeni
 Wananchi wakinyoosha mikono ikiwa ni ishara ya kukubali kumpigia kura ya ndiyoi Godfrey Mgimwa siku ya uchaguzi Machi 6, mwaka huu.
 Kila mara ilikuwa ni furaha
Mgimwa akiongozwa na wanakijiji wenzie
 Wakiwa wamesimama kwa muda wa dakika moja kumuombea marehemu Dk. William Mgimwa
Bibi yake Godfrey Mgimwa , Consolata Semgovano akitoa neno la baraka kwa mjukuu wake ili ashinde uchaguzi huo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

CRDB yazindua huduma ya malipo ya gharama za matibabu kwa njia ya Kadi KCMC


Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa tawi dogo la CRDB pamoja na uzinduzi wa utolewaji wa huduma ya malipo ya gharama za matibabu kwa njia ya Kadi katika hosptali ya rufaa ya KCMC.
Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheli dayosisi ya kaskazini,Dk Martin Shao akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi dogo la CRDB pamoja na uzinduzi wa utolewaji wa huduma ya malipo ya gharama za matibabu kwa njia ya Kadi katika hosptali ya rufaa ya KCMC.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa katika viwanja vya hosptali ya rufaa ya KCMC kufuatilia uzinduzi huo.
Wachungaji wakishirikisha neno la Mungu wakati wa hafla ya katika hosptali ya rufaa ya KCMC ya uzinduzi wa tawi dogo la CRDB pamoja na uzinduzi wa utolewaji wa huduma ya malipo ya gharama za matibabu kwa njia ya Kadi katika hosptali ya rufaa ya KCMC.
Baadhi ya mameneja na wafanyakazi wa CRDB wakifuatilia hafla hiyo.
Tawi dogo la Benki ya CRDB lililozinduliwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC.
Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheli dayosisi ya kaskazini Dk Martini Shao akiwa na mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB Dk Charles Kimei pamoja na wageni wengine mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja wakionesha kadi ya mfano ya kulipia gharama za matibabu katika hospitali ya rufaa ya KCMC.
Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheli dayosisi ya kaskazini Dk Martini Shao akiwa na mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB Dk Charles Kimei wakielekea katika jengo la tawi dogo la Benki ya CRDB kwa ajili ya uzinduzi.

Burudani ya ngoma ilikuwepo kwa ajili ya wageni waalikwa.
Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheli dayosisi ya kaskazini Dk Martini Shao akiwa na mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB pamoja na kaimu mkurugenzi wa hosptali ya KCMC .Prof Raimosi Ollomi wakati akizindua tawi dogo la Benki ya CRDB.
Mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB,Dk Charles Kimei akimuelekeza jambo Askofu Dk Martin Shao kabla ya uzinduzi wa huduma ya malipo ya gharama za matibabu kwa njia ya Kadi.

Askofu Dk Martini Shao akizindua rasmi huduma ya malipo ya gharama za matibabu kwa njia ya Kadi ambayo sasa itatolewa katika hospitali ya rufaa ya KCMC.

Mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB Dk Charles Kimei akifanya malipo kwa njia ya kadi katika hospitali ya rufaa ya KCMC ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma hiyo. Picha na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,Moshi.